NYOTA
wa Bongo Fleva na Bosi wa lebo ya Poz kwa Poz ‘PKP’, Omary Nyembo ‘Ommy
Dimpoz’, amesema moja ya matukio ambayo hawezi kuyasahau ni siku
aliposwekwa lupango huko Marekani kwa kosa la kutumia vibaya hati yake
ya kusafiria.
Akibonga na Swaggaz hivi karibuni, Ommy Dimpoz,
alisema alikuwa anatokea Uingereza kwenda Marekani, viza aliyokatiwa na
promota wake ilikuwa ni ya kwenda kutalii na siyo kufanya kazi kama
mwenyeji wake huyo alivyo mdanganya.
“Nilipofika uwanja wa ndege
nilishangaa kuambiwa nisubiri kwenye chumba tofauti na wenzangu.
Nikaanza kuhojiwa nitoe sababu za kuingia Marekani, mimi nikasema
nimekwenda kutembea.
Wakaomba mawasiliano ya mwenyeji wangu,
nikawapa ya promota, sijui waliongea naye nini ila yule ofisa wa uwanja
wa ndege aliporudi kwenye chumba kile alikuja na askari polisi wawili na
akaniambia nimedanganya nakwenda kutembea wakati nakwenda kufanya kazi
kitu ambacho ni kosa, kwa hiyo nikawekwa chini ya ulinzi,” alisema
Dimpoz.
Ommy Dimpoz, anasema baada ya kutiwa nguvuni, akavishwa
mavazi ya jela, akapigwa pingu na kupelekwa jela ambako aliyafurahia
maisha ya kule kutokana vyakula vitamu wanavyopewa wafunga na baada ya
hapo alirudishwa Tanzania.
Mtanzania
-
Blogger Comment
-
Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments :
Post a Comment